Back to top

Mwanafunzi amkata panga mwalimu kukwepa adhabu ya utoro.

24 September 2020
Share

Mwanafunzi wa kidato cha Tatu cha katika shule ya sekondari ya Kiagata wilayani Butiama mkoani Mara Mwita Juma Machango amemjeruhi kwa panga mkono wa kushoto mwalimu wake Majogoro John, baada ya kupewa adhabu kutokana na utoro.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mara Joachim Eyembe amethibitisha kumpokea mwalimu huyo ambaye amepelekwa kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Daniel Shillah ambaye amethibitisha tukio hilo, amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanafunzi huyo kwa hatua za kisheria.