Back to top

MWANAFUNZI WA MIAKA 6 AMPIGA RISASI MWALIMU MAREKANI

08 January 2023
Share

Mwanafunzi wa kiume mwenye umri wa miaka sita ,anashikiliwa na polisi baada ya kumpiga risasi mwalimu wa Shule ya Msingi ya Richneck, katika jiji la Newport News, huko Virginia nchini Marekani.

Tukio hilo lilitokea katika chumba cha darasa la kwanza chenye wanafunzi wa umri wa miaka sita hadi saba, baada ya kutokea ugomvi kati ya wawili hao.

Mkuu wa Polisi wa eneo hilo Steve Drew, amesema haijulikani ni jinsi gani mtoto huyo aliipata bunduki hiyo, lakini Bwana Drew amesema tukio hilo halikuwa la bahati mbaya, na mwalimu huyo ambaye hakutajwa jina na anasemekana kuwa na umri wa miaka 30 amepata majeraha makubwa.

Polisi wamekataa kutaja silaha iliyotumika katika tukio hilo, lakini wamesema kijana huyo alitumia bunduki.