
Gabriel Okedi (38), ambaye ni Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF), anashikiliwa na Polisi nchini Uganda, akituhumiwa kumpa ujauzito binti yake mwenye umri wa miaka 15.
.
Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Polisi Mkoa wa Ssezibwa, nchini humo, Hellen Butoto, amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Njeru, akisubiri kuchukuliwa hatua za kisheria.