Back to top

Mwanaume adaiwa kuuawa na mume wa mpenzi wake.

22 June 2022
Share

Mkazi wa kijiji cha Kiziwa  Kata ya Kiroka wilayani Morogoro Kibwana Mussa amekutwa ameuawa kwa kukatwa mapanga nyumbani kwa mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kiziwa, Mbena Loki alisema kuwa mkazi huyo aliuawa na mtu aliyedaiwa kuwa ni mume wa mwanamke aliyemtaja kwa jina la Farida Ally.