Back to top

Mwandishi wa Aljazeera auawa akiwa kazini.

11 May 2022
Share

Mwandishi wa habari wa Al Jazeera Shireen Abu Akleh (51) ameuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa akiwa katika majukumu yake ya kazi ya kufuatilia uvamizi wa Jeshi la Israel kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin, Palestina.

Al Jazeera imevishutumu vikosi vya usalama vya Israel kwa kumlenga na kumuua kwa makusudi Abu Akleh na kuitaka jumuiya ya kimataifa kulaani na kuiwajibisha Israel.

Mwandishi mwingine wa habari wa Palestina, Ali al-Samoudi pia alijeruhiwa mgongoni lakini hali yake inaendelea vizuri.


Jeshi la Ulinzi la Israel limedai kuwa vikosi vyake vya usalama vimekuwa vikifanya kazi katika eneo hilo kuwakamata washukiwa wa matukio ya kigaidi," na washukiwa wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel wote walikuwa wakifyatua risasi wakati huo.