Back to top

Mwandishi wa Habari wa ITV, Gabriel Kandonga afariki dunia.

24 September 2021
Share

Mwandishi wa Habari wa ITV na Radio One wa mkoani Songwe Gabriel Kandonga amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea asubuhi ya leo wakati akitokea Wilayani Tunduma kwenda wilayani Songwe akielekea kwenye majukumu ya kikazi.
.
Mkuu wa mkoa wa Songwe Omary Mgumba amesema Kandonga amefariki baada ya gari alilokuwa akiendesha kwenye barabara kuu ya Tunduma-Songwe kuligonga gari jingine ambalo lilikuwa limeegeshwa kwa kuwa lilikuwa bovu.
.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa Mkoa, Kandonga na Mwanahabari mwenzie wa Clouds TV Aika Sanga ambaye alijeruhiwa walikuwa wakienda katika kufanya majukumu yao ya habari kwenye kamati ya bunge  ya masuala ya ukimwi ambayo ipo wilayani Songwe.
.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema peponi.