
Bodi ya Sukari nchini kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, imefanya operesheni na kuwakamata wafanyabiashara watano wa maduka ya jumla na rejareja baada ya kubainika kuwa wanauza kilo moja ya sukari kwa shilingi 4000 hadi 5000, tofauti na bei elekezi ya serikali ya shilingi 2,800/= hadi 3,000/=.
.
Akizungumza baada ya operesheni hiyo, Afisa kutoka Bodi ya Sukari, ambaye ndiyo aliyeongoza oparesheni hiyo, Bw.George Gowele, amesema operesheni hiyo ililenga kuwabaini na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaoendelea kukiuka bei elekezi.
.
Bw.Gowele amesema licha ya serikali kufuta ushuru wa kuingiza sukari nchini lakini bado baadhi ya wafanyabishara wameendelea kukiuka bei elekezi iliyopangwa na serikali hivyo kuendelea kusababisha ugumu wa upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa walaji.
