Back to top

MWENYEKITI IEBC ASEMA MATOKEO YA KURA HAYAWEZI KUBADILISHWA

10 August 2022
Share

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) Bwana Wafula Chebukati, amesema matokeo ya kura yaliyotangazwa kwenye vituo vya kupigia kura ndiyo ya mwisho, na kwamba hayawezi kubadilishwa na mtu yeyote.

Katika hotuba yake kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Bomas, Bwana Chebukati amesema zoezi la upigaji kura lilimalizika vyema katika vituo vingi na kwamba vituo 26,881 kati ya 46,229 kote nchini vimemaliza kuhesabu kura na kutuma fomu zake hadi Bomas.

Bwana Chebukati amesema Siku ya kupiga kura kwa kiasi kikubwa ilikuwa ya amani, lakini wapiga kura waliojitokeza walikuwa wachache na tume hiyo inakadiria waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 60%, ikiwa ni idadi ya chini ikilinganishwa na asilimia 80% iliyoonekana katika uchaguzi mkuu uliopita.

Kadhalika bwana Chebukati amesema zoezi linaloendelea ni la kuhesabu kura kwa umakini ili kutekeleza takwa la kisheria la kutangaza matokeo ndani ya siku saba.