Back to top

MWILI HAYATI ALI HASSAN MWINYI KUAGWA UWANJA WA UHURU

01 March 2024
Share

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa, ametangaza ratiba ya maziko ya Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, itakayoanza leo Machi 01, 2024.
.
Waziri Mkuu amesema mwili utaondoka nyumbani kwa Hayati Mwinyi  saa 5:30 Asubuhi, kuelekea Msikiti Mkuu wa BAKWATA Kinondoni ambapo Sheikh Dkt. Abubakar Bin Zuber Bin Ali, ataongoza swala ya Ijumaa na taratibu zote za kidini.
.
Saa 8:00 Mchana, mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, utaelekea Uwanja wa Uhuru na kwamba kuanzia saa 8:30 mchana ni dua na maombi kutoka kwa Viongozi wa Dini, pamoja na Viongozi mbalimbali na Wananchi kutoa heshima za mwisho.
.
Saa 11:00 jioni mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, utaondolewa uwanja wa Uhuru kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, na saa 11:30 Jioni Wananchi wa Zanzibar na maeneo mengine ya Unguja wataupokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume.