Back to top

Mwili waokotwa kwenye kiroba Dar es salaam.

16 January 2019
Share

Mwili wa mtu mmoja umeokotwa eneo la sayansi jirani na Chuo cha Ustawi wa jamii ukiwa umefungwa kwenye kiroba. 
 
ITV imefika katika eneo hilo na kushuhudia kiroba hicho ambacho baadae kilichunguzwa na maafisa usalama na kugundua ni mwili wa binadamu. 
 
Mjumbe wa mtaa huo Bi Fortunata Mshindo akizungumza na ITV amesema mchana yeye na wananchi wengine walipita katika eneo hilo na hakukua na kitu chochote huku pia akisisitizia uongozi wa manispaa kuweka taa katika eneo hilo ili kupunguza matukio ya kihalifu.