
Rais wa Zanzibar, Mhe.Dkt.Hussein Ally Mwinyi ameondoka Zanzibar kuelekea Havana nchini Cuba, ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la 77 na China (G77+ China), unaotarajiwa kufanyika Septemba 15 na 16, 2023.

