Back to top

Magufuli awataka Mawaziri kufanya kazi kwa bidii kukidhi matarajio.

16 November 2020
Share

Rais Dakta John Pombe Magufuli amemuapisha Waziri Mkuu Mteule Mheshimiwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wengine walioapishwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mteule Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Fedha na Mipango mteule Dakta Philip Mpango kuwa mawaziri.

Baada ya kuapishwa kila mmoja wao aliahidi kufanya kazi kwa uadilifu na kumshauri Rais kutekeleza majulumu yake kwa mujibu wa katiba.

Kwa upande wake Rais Magufuli amewataka mawaziri hao wakafanye kazi kwa bidii ili kukidhi matarajio ya wananchi waliowachagua kwa kura nyingi kupitia Chama Cha Mapinduzi.