Back to top

MWINYI: BABA ALINIAGIZA NIWE MSIMAMIZI WA FAMILIA

03 March 2024
Share

Rais wa Zanzibar, Mhe.Hussein Ali Mwinyi, amesema Baba yake, Hayati Ali Hassan Mwinyi aliwaita yeye na ndugu zake na akawataka kuunda udugu kati yao ambapo alimtaka yeye awe msimamizi wa ndugu zake.
.
Mhe.Dk. Hussein Mwinyi ameyasema hayo leo, kwenye hitma ya kumuombea Hayati Mzee Mwinyi, iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, vilivyopo mkoani Mjini Magharibi, Unguja.
.
"Mzee alitoa wosia, alituita siku moja akatuambia nyinyi vijana wangu, siku zilizobaki kwangu si nyingi, kwa hivyo nakuombeni muunge udugu na akanitaka mimi kwa jina, akasema Hussein nakuagiza wewe utakuwa msimamizi wa familia, si kwa sababu wewe ni mkubwa wapo wakubwa zako, lakini kwa sababu ya wadhifa uliokuwa nao nawaweka ndugu zako hawa chini ya mwongozo wako" Alisema Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi
.
Aidha, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa bega kwa bega tangu Baba yake, Hayati Ali Hassan Mwinyi, alipoanza kuugua mnamo mwezi Novemba, alipopelekwa Uingereza kwa matibabu.