Back to top

MWINYI:SERIKALI KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA ELIMU

30 July 2022
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dakta Hussein Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwekeza katika vyuo vya Mafunzo ya Amali kwa wanafunzi ambao hawakupata nafasi ya kuendelea.

Aidha, amesema serikali itawapatia mikopo ya elimu ya juu katika bodi zote mbili ikiwemo ile ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jambo ambalo litawawezesha kujiendeleza kielimu.

Ametoa ahadi hiyo katika Ikulu ndogo ya Pagali Kisiwani Pemba, katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa Kidato cha Nne 2021 na Sita waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kitaifa ya mwaka 2022 na kula nao chakula kwa pamoja alichowaandalia.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwekeza katika sekta ya elimu, ili wanafunzi wapate mazingira mazuri ya kusoma na kufanya vyema katika mitihani yao.

Katika kuzithamini juhudi za wanafunzi hao, Rais Mmwinyi ametoa nafasi za udhamini wa masomo kwa wanafunzi thelathini waliofanya vizuri katika mitihani yao ili kuendelea na masomo katika vyuo mbali mbali.