Back to top

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa amewasili nchini kwa zaiara.

11 September 2021
Share

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa Mhe. Amina Mohammed amewasili nchini kwa zaiara ya ya siku mbili kuwasilisha ujumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Antonio Guteres kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Mhe Amina Mohamed amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.