Back to top

Naibu Spika atoa ufafanuzi kulipuka kwa moto.

10 April 2018
Share

Naibu spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansansu amesema moshi uliotanda jana ndani ya ukumbi wa Bunge ulitokana na kulipuka kwa mashine ya kuchajia simu maarufu kama “Power Bank” iliyokuwa ikichaji simu mbili kwa mkupuo ndani ya ukumbi wa Bunge.

Naibu Spika amesema mashine hiyo ilikuwa ikimilikiwa na mmoja kati ya wabunge ambaye alikuwa amekaa upande wa kulia wa kiti cha spika wa Bunge 

Naibu Spika amesema kutokana na moshi huo mwenyekiti wa Bunge Mhe.Musa Azzan Zungu alilazimika kuhahirisha kikao cha Bunge. 

Jana saa moja na nusu usiku moto ulitanda ndani ya ukumbi wa Bunge Dodoma na kuzua taharuki ambayo baadhi ya wabunge walikimbilia nje ya ukumbi huo na umeme kukatika takribani dakika 6 mkoani Dodoma