Back to top

NAIBU WAZIRI MKUU WA CHINA ATEMBELEA TAASISI YA JKCI

22 January 2024
Share

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Liu Guozhong ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku Tatu, ametembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na amepokelewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel.
.
Mhe. Guozhong ametembelea Chumba cha upasuaji mdogo wa moyo, chumba cha wagonjwa wa moyo wanaohitaji uangalizi maalum na chumba cha uangalizi maalum kwa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo.


Dkt. Mollel amesema kuwa ziara ya Mhe. Mhe. Guozhong nchini Tanzania ni sehemu ya mahusiano mazuri baina ya Tanzania na China, pamoja na kujionea mapinduzi makubwa yaliofanywa na Mhe.Rais  Samia Suluhu Hassan katika kuwekeza kwenye sekta ya afya hususani Tiba Utalii.
.
“Ushirikiano wetu na China ni kubadiulishana ujuzi katika kutoa Huduma kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kujitanua zaidi eneo la Tiba Utalii”, alisema Dkt. Mollel.