Back to top

Naibu waziri aufunga mgodi ulioua watano Gairo.

09 June 2019
Share

Watu watano ambao ni wanaume wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi wakichimba madini aina ya dhahabu huku wengine watano wakijeruhiwa katika mgodi wa Kirama uliopo kata ya Kiogwe wilayani Gairo mkoa wa Morogoro na kusababishwa kufungwa kwa mgodi huo ambao ulikuwa haujafunguliwa rasmi.


Naibu Waziri wa madini mheshimiwa Stanslaus Nyongo amefika katika tukio hilo na kutoa pole kwa waliopoteza maisha huku akilazimika kuufunga mgodi huo hadi taratibu za kisheria zifuatwe ndipo taratibu za uchimbaji zianze.


Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro kamishina mwandamizi wa polisi sacp wilbroad mutafungwa akathibitisha kutokea kwa vifo hivyo.