Back to top

Naibu Waziri Gekul:Siri ya maisha ya sasa ni kutenga muda wa mazoezi.

01 August 2022
Share

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Pauline Gekul , amesema kuwa kwa miaka ya sasa ya magongwa yasiyoambukiza, siri ya maisha ya afya njema ni kujitengea muda wa kufanya mazoezi wewe mwenyewe,  ili uwe salama na afya yako.

Naibu Waziri Mhe. Gekul amesema hayo akiwa Mji Mkongwe wa Bagamoyo wakati anafunga mashindano ya mbio za Bagamoyo Marathon zinazoandaliwa na Kampuni ya For Better Life (4 Bel) zikihusisha wanariadha kwa mbio za km 21, km 10 na Km 5 amabazo yeye mwenyewe alishiriki kuanzia mwanzo hadi mwisho.

 
"Natoa rai kwa Watanzania kupitia mbio za Babamoyo marathon, kwamba Watanzania tutenge muda wa kufanya mazoezi, Mhe. Rias Samia Suluhu Hasaan alisema kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, nawahimiza wananchi wote tuendelee kufanya mazoezi katika maeneo yenu, maafisa michezo kote nchini msimamie vikundi vya jogging kwenye maeneo yenu kwa kuhamasisha kupitia nyimbo za kizalendo ili kuwavuta watu wengi kushiriki kufanya mazoezi".Naibu Waziri Mhe. Gekul 

Aidha, amezipongeza familia zilizojitokeza kushiriki mbio za Bagamoyo Marathon ikizingatiwa baba na mama wanaopenda familia zao, siri ya sasa ili ufikie umri wa wazee wetu ni muhimu kujitengea muda wa mazoezi na wanafamilia.

Akiongea wakati akimkaribisha Naibu Waziri Mhe. Gekul, Mkurugenzi wa Kampuni ya For Better Life (4 Bel) Dkt. Deogratius Soka amesema mbio hizo zinalengo la kuongeza chachu na kutia hamasa katika mchezo wa riadha nchini na kuongeza ajira kwa vijana, kukuza utalii ikizingatiwa mji huo unahistoria ndefu ya Taifa hili, kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi pamoja na kutoa burudani na kuondoa msongo wa mawazo kwa Watanzania na watu wengine wanaoshiriki mbio hizo.