Back to top

NAIBU WAZIRI KUNDO AKAGUA VIFAA VYA MNARA LUDEWA.

28 November 2022
Share

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew amekagua vifaa vya ujenzi wa mnara wa mawasiliano utakaojengwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Tigo katika Kijiji cha Nkwimbili Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe.
 
Naibu Waziri Kundo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano, wakati wa ujenzi wa mradi huo pamoja na kuulinda mara utakapoanza kutoa huduma, huku akiwasii kutumia vizuri fursa za mawasiliano watakazopata kutokana na mnara huo.

“Ifikapo Januari 2023 mnara huu utaanza kutoa huduma kwa wananchi, na hivyo kutatua changamoto ya mawasiliano katika eneo hili. Wizara tuna miradi ya mipakani na maeneo maalum ili kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano kutoka nchini kwanza ikiwa ni pamoja na kuchangia uchumi wa nchi kwa manufaa yetu sote”, Mhe. Naibu Waziri Kundo.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa mnara katika Kijiji cha Nkwimbili kutoka Kampuni ya GNC Solutions LTD, Bw. Suleiman Senga ameahidi kuwa mnara huo utaanza kutoa huduma ifikapo Januari 2023 na kuwa kampuni zingine za simu zinaweza kutumia mnara huyo wa Kampuni ya Tigo kutoa huduma kwa wananchi kupitia kampuni zao.

Katika hatua nyingine, Mhe. Naibu Waziri Kundo ameielekeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha kuwa wanazingatia utaratibu na kuzisaidia kupata leseni kwa haraka redio mbalimbali zilizowasilisha maombi yao ikiwa ni pamoja na redio za halmashauri.