Back to top

Naibu Waziri Mabula ataka wadaiwa sugu kodi ya ardhi kubanwa.

18 May 2020
Share

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinapeleka hati za madai ya kodi ya pango la ardhi kwa wadaiwa sugu wa kodi hiyo kuanzia Jumatatu tarehe 18 Mei 2020 na watakaokaidi kulipa kwa hiari wafikishwe kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba ya Wilaya.

Dkt Mabula alitoa maagizo hayo akiwa katika ziara yake mkoani Iringa kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi sambamba na kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika baadhi ya Taasisi zilizopo katika halmashauri za Manispaa na wilaya ya Iringa.


Dkt Mabula alizitaka idara za ardhi katika halmashauri zote nchini kupitia kumbukumbu za wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi vizuri na kuwaandikia Hati za Madai zitakazowataka wadaiwa kulipa kwa hiari madeni yao na watakaokaidi wafikishwe katika Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba ya Wilaya.