Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Pinda, ametaka kuwepo upendo miongoni mwa watumishi, ili waweze kutekeleza majukumu kwa ufanisi.
Mhe.Pinda ameeleza hayo Jijini Dodoma, wakati alizingumza na viongozi na watumishi wa Wizara ya Ardhi Makao makuu na kuwataka watumishi hao wa sekta ya ardhi kufanya kazi kwa bidii ili serikali ione matunda na ufanisi wa kazi walizotumwa kuzitekeleza.
Amesema upendo miomgoni mwa watumishi siyo tu unatoa faraja kwa watumishi bali unarahisisha kazi za wizara kwa kuwa watumishi hao watakuwa wakifanya kazi kwa furaha na amani.
Amebainisha kuwa, uamuzi wa kukutana na watumishi unalenga pia kuwafunda na kuwaweka karibu watumishi ili wizara ya ardhi ifanye kazi kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya.
Pia Mhe.Pinda ametaka watumishi wa sekta hiyo kupewa stahiki zao kwa mujibu wa sheŕia, taratibu na miongozo iliyopo ili wafanye kazi kwa bidii bila manung'uniko.