
Waziri wa Habari na Mawasiliano, Mhe.Nape Nnauye, ameielekeza Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), kuruhusu ubunifu kwenye tasnia ya Habari.
.
Maelekezo hayo yamefuata siku moja baada ya Mamlaka hiyo kuzuia usomaji wa magazeti kwa mbembwe, ambapo amebainisha kuwa staili mbalimbali za usomaji magazeti zimeongeza mvuto kwenye usomaji wa magazeti, hivyo jambo hilo ni la kutiwa moyo na sio kuzuiliwa.
.
Mhe.Nape ametoa maelekezo hayo kupitia mtandao wa X.com, ambapo pia ameitaka Mamlaka hiyo, kujenga utamaduni wa kuzungumza kabla ya kuagiza.
