Back to top

NATO YAWEKA MSIMAMO WAKE KUJITOLEA KATIKA SUALA LA UKRAINE

30 November 2022
Share

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami (NATO) Jens Stoltenberg, amethibitisha tena msimamo wa muungano huo wa kijeshi wa kujitolea katika suala la Ukraine, akisema nchi hiyo siku moja itakuwa mwanachama wa jumuiya hiyo kubwa ya kiusalama duniani.

Amesema kwamba milango ya NATO iko wazi kwa kuikubalia hivi karibuni, Montenegro na Macedonia kaskazini kuwa wanachama, licha ya upinzani mkali wa Urusi kuonesha kwamba nchi hiyo haina kura ya turufu.

Kauli ya Katibu Mkuu huyo wa Nato imekuja wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken pamoja na wenzake kutoka jumuiya hiyo wakikusanyika nchini Romania kwa ajili ya kuimarisha msaada wa dharura unaohitajika nchini Ukraine.

Uungaji mkono huo wa NATO, unalenga kuhakikisha kwamba Urusi inashindwa kuiangusha Ukraine katika wakati ambapo inaendelea kushambulia miundo mbinu ya nishati ya nchi hiyo.