
Kiongozi mkuu wa upinzani aliye kizuizini nchini Urusi, Alexei Navalny, ameishutumu serikali ya nchi hiyo kwa kutumia gereza kudhoofisha afya yake.
Navalny ameandika ujumbe wake kupitia mtandao wa Twitter kuwa amekuwa na maumivu ya muda mrefu mgongoni yanayosabishwa na kusimama kwa muda mrefu gerezani, hali ambayo ambayo ameitaja kuwa sehemu ya mkakati wa makusudi wa mamlaka kudhoofisha afya yake.
Navalny ameeleza kuwa aliomba kwa mwezi mmoja na nusu kuonana na daktari lakini alipokuja alimfanyia uchunguzi kwa dakika tano tu, na kukataa kumwambia alichokua anaugua.
