
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imesema kutakuwa na mabadiliko ya ratiba za safari zake za China, kutokana na ndege zake mbili za masafa marefu, Boeing 787-7 (Dreamliner) kufikia muda wake wa matengenezo ya kawaida (mantainance schedule).
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo imesema kuwa matengenezo hayo yalipangwa kufanyika kwa awamu, lakini kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa ugavi katika utengenezaji wa vipuri vya ndege uliosababishwa na athari za UVIKO-19, matengenezo hayo yamepangwa kufanyika kwa pamoja ili kuondoa hatari ya kukosekana kwake kwa muda mrefu.