Back to top

NDEGE ZA KIMATAIFA, KUPAISHA UTALII WA TANZANIA.

31 May 2024
Share

Mashirika ya ndege ya Kimataifa ya Qatar Airways, Emirates na Turkish Airlines kutangaza vivutio vya utalii vivanvyopatikana nchini Tanzania.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki akieleza vipaumbele vya wizara alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 jijini Dodoma.

Aidha Mhe. Kairuki amesema Wizara itaendelea kutangaza utalii ndani na nje ya nchi, kupitia matangazo katika Ligi na Mashindano ya Michezo yenye wafuatiliaji wengi zaidi Duniani, kutumia watu mashuhuri na wenye ushawishi, Mabalozi wa hiari wa utalii, vyombo vya habari vya Kimataifa vyenye ushawishi.

Aidha,  Mhe. Kairuki aliongeza kuwa Wizara itaendelea kukamilisha taratibu za kujitangaza kupitia Ligi za Michezo mikubwa duniani za Marekani na Uingereza na Matukio makubwa ya Burudani.