
Urusi imepiga marufuku Mashirika ya ndege ya Uingereza kutua katika viwanja vya ndege vya Urusi pamoja na kupita kwenye anga lake baada ya Uingereza kupiga marufuku Shirika la Ndege la Urusi, Aeroflot kutua nchini Uingereza ikiwa ni moja ya vikwazo vilivyowekwa ili kukabiliana na Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
