Back to top

NDERIANANGA AGAWA MITUNGI YA GESI KWA WALEMAVU

02 August 2023
Share

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga, ametoa mitungi ya gesi kwa watu wenye ulemavu na vikundi vya wanawake, ikiwa ni moja ya jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.
.
Mhe.Nderiananga ametoa mitungi hiyo, wakati akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, ambapo ameitaka jamii kutumia nishati mbadala na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, ili kulinda afya zao na mazingira.
.
"Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan anatoa fedha nyingi katika maeneo mengi ikiwemo programu ya kumtua mama ndoo kichwani lakini akasema wakina mama wanapata shida wao ndio wapishi sasa ni wakati wa kuwatua kuni kichwani kwa kuwasaidia kupata nishati ya gesi na mimi nimekuja kutekeleza adhma yake ya kumtua mama kuni kichwani” Amesema Mhe.Ummy