Back to top

NDUGAI ANG'ATUKA USPIKA WA BUNGE.

06 January 2022
Share

Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai ameandika barua ya kujiuzulu nafasi ya Uspika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo katika barua hiyo amesema amechukua uamuzi huo kwa hiari yake kwa kuzingatia na kujali maslahi mapana zaidi ya Taifa, Serikali na Chama chake cha Mapinduzi (CCM).

Barua ya Ndugai ya Kujiuzulu ameielekeza kwa Katibu Mkuu wa CCM na Katibu wa Bunge.