Back to top

Ndugai aongoza kikao cha Bunge Dodoma

09 April 2018
Share

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe.Job Ndugai leo ameongoza kikao cha tano cha mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ikiwa siku chache tangu awasili nchini kutoka katika matibabu nchini India.

Mara baada ya Spika kuingia Bungeni hapo kuongoza wabunge walionesha furaha yao kumuona kufuatia kutoonekana kwake Bungeni tangu Mwezi Novemba mwaka jana na kutoonekana kabisa katika mkutano uliopita wa bunge.

Spika Ndugai amesema amepitia kipindi kigumu cha matibabu na anashukuru jinsi ambavyo Mwenyezi Mungu kwa jinsi alivyopambania maisha yake sambamba na ushirikiano aliopata kutoka Serikalini na Bungeni.

Amesema kwa sasa ameimarika kiafya na yupo sawa kuongoza shughuli mbalimbali za Bungeni hapo