Back to top

Ndungulile ataka mama aliyenunua Drip kwa pesa yake kurudishiwa.

23 July 2018
Share

Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndungulile ameuagiza uongozi wa hosptali ya mkoa wa Simiyu kumrudishia mara moja pesa zake mama mmoja mkazi wa bariadi ambaye amelazwa katika wodi ya watoto baada ya kumueleza waziri kuwa aliambiwa na manesi kuwa akanunue maji kwa ajili ya kumtundikia mwanae ambaye anaumwa.

Dkt.Ndungulile ametoa Kauli hiyo wakati alipotembelea hospitali hiyo na kuonana na wagonjwa mbalimbali ambapo akiwa katika wodi ya watoto alimuuliza mama huyo kuhusu huduma alizopata na mwanae ambaye pasipo kuficha alimuambia kuwa aliambiwa akanunue maji ya Drip kwa pesa yake katika maduka ya nje.

Aidha Naibu Waziri huyo ameuagiza uongozi wa mkoa Simiyu kuwatafuta watu wanaoishi na VVU waliocha kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi zaidi ya elfu kumi pamoja na ongezeko la vifo vya wakinamama wajawazito ambapo pia ametaka kufahamu mikakati ya mkoa katika kuangalia tatizo la idadi kubwa watu wanaokatisha dawa za kurefusha maisha ili waweze kukabiliana nalo.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kuwahimiza wananchi kupima kwa hiari VVU ili mkoa uweze kutokomeza kabisa ugonjwa huo.