Back to top

NEC kuwachukulia hatua wasimamizi watakao haribu uchaguzi.

17 October 2020
Share

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema itawachukulia hatua za kisheria wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo na kata watakaoharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, hivyo imewataka wasimamie sheria na taratibu za uchaguzi, ili kuepuka kuiingiza nchi kwenye machafuko.

Mkurugenzi wa tume hiyo Dkt.Wilson Mahera ametoa onyo hilo mjini Songea alipozungumza na wasimamizi wa uchaguzi kutoka mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Lindi na Mtwara kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi, ili uchaguzi ufanyike kwa amani.

Dkt.Mahera amesema vituo vya kupigia kura vimeongezeka kilinganishwa na vile vya mwaka 2015.

Wakati huo huo Kamishna wa tume hiyo Jaji Mstaafu Thomas Mihayo mewahadharisha waratabu na wasimamizi wa uchaguzi kuwa watalazimika kufidia gharama za uchaguzi wa marudio endapo watasababisha matokeo yatenguliwe na mahakama.

Aametoa hadhari hiyo jijini Mwanza alipozungumza na waratibu na wasimamizi wa uchaguzi kutoka mikoa mbalimbali.

Wasimamizi na waratibu hao wa uchaguzi wamekutana na tume hiyo ili kukumbushana masuala muhimu ya kufanikisha uchaguzi mkuu.

Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amewasisitiza wazingatie maelekezo ya ujenzi wa vituo vya kupigia kura.

Pia Tume hiyo ya Uchaguzi NEC imesema taasisi tisini na saba za hapa nchini na kumi na saba za nje zimekidhi vigezo vya kuwa waangalizi kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kwa upande wake Kamishna wa tume hiyo Asna Omari ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya waangalizi watakaofanya kazi hiyo yaliyoandaliwa na Kituo cha Kimataia cha Sera barani Afrika.

Mwenyekiti wa bodi ya kituo hicho Profesa Rwekaza Mukandara amesema waangalizi hao watafanya kazi hiyo kama tume ilivyoelekeza na siyo vinginevyo.