Back to top

NEC yawataka wananchi kuhakiki taarifa zao kabla ya muda wa mwisho.

19 June 2020
Share

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wananchi kwenda kwenye vituo walivyojiandikishia kuhakiki taarifa zao kwenye Daftari la Mpiga Kura wakati huu wa zoezi la uwekaji wazi wa daftari la awali la awamu ya pili ambalo ukomo wake ni 20 Juni,2020.

Afisa Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bi.Nuru Riwa amesema zipo njia nne za kuhakiki taarifa kwa mpiga kura ikiwemo kwa njia ya simu *152*00#, kutembelea tovuti nec.go.tz au kupiga huduma kwa wateja 0800112100.