Back to top

NECTA yatangaza kuanza kwa mtihani wa Kidato cha sita na Ualimu

28 June 2020
Share

Baraza la mitihani Tanzania limetangaza kuanza mtihani wa kidato cha sita na ualimu kesho jumatatu huku likitoa wito kwa wasimamizi kufanya kazi yao kwa uadilifu wa hali ya juu na kuzitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha taratibu zinazingatiwa.

Akizungumzia mtihani huo Katibu wa Baraza hilo Dkt.Charles Msonde amezitaka kamati hizo kuhakikisha taratibu za uendeshaji mitihani zinazingatiwa kudhibiti mianya ya udanganyifu.

Dkt.Msonde amewataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yeyote kuingilia majukumu ya wasimamizi.

Jumla ya watahiniwa 85,546 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita 2020 ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 74,805 na watahiniwa wa kujitegemea ni 10,741
Kati ya watahiniwa wa shule 74,805 waliosajiliwa wanaume ni 42,284 sawa na asilimia 56.53 na wanawake ni 32,521 sawa na asilimia 43.47.

Kwa upande wa watahiniwa wenye uhitaji maalum wapo 113 na Kati Yao 72 Ni wenye uoni hafifu ,19 wasioona na 19 wenye ulemavu kusikia na watatu wenye ulemavu wa akili.