Back to top

NEC:Wanahabari epukeni habari zenye ukakasi.

15 September 2020
Share

Tume ya Taifa ya uchaguzi( NEC) imewataka wanahabari hususani wa mitandao ya kijamii kuhakikisha taarifa wanazozitoa zinakuwa zenye mashiko kwa jamii na ambazo hazimkashfu mtu wala kuegemea upande wowote, kwani mitandao ya kijamii imekuwa jukwaa kubwa la kuhabarisha umma hivyo kama kuna taarifa ambayo inaukakasi ni vyema kupata taarifa sahihi kutoka kwenye tume hiyo ya uchaguzi.

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC Dkt.Charles Mahera akiongea na waandishi wa Habari za mitandao ya kijamii katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere Dar es Salaam amesisitiza kuwa ni vyema wanahabari kutumia kalamu zao kuandika habari ambazo zitaleta matokeo chanya.

NEC imesema licha ya mitandao kuwa jukwaa kubwa katika kuuhabarisha umma lakini waendeshaji wake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya mpiga kura lakini vilevile nawaopaswa kupata elimu hiyo kwa kina kusudi.