Back to top

NFRA yaiuzia mahindi zaidi ya tani elfu thelathini na sita WFP.

10 February 2019
Share

Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) umeingia mkataba wa kuliuzia mahindi shirika lisilo la kiserikali la mpango wa chakula duniani (WFP) kiasi cha tani elfu 36 ambazo zinasafirishwa na kupelekwa kwenye nchi zenye uhaba wa chakula ikiwemo  Uganda na Sudani Kusini.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa zoezi la kupakia mahindi kwa ajili ya kusafirisha kama sehemu ya msaada kwa wakimbizi na mataifa yaliyoathiriwa na vita Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Bi.Vumilia Zikankuba amesema (WFP) mpaka sasa imekwishachukua zaidi ya tani elfu kumi na tano za mahindi ambapo amesema wamekuwa wakisafirsha mahindi kupitia njia ya reli na barabara.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha usafirishaji cha mpango wa chakula duniani (WFP) Mahamudu Mabuyu amesema mahindi hayo yanasafirshwa kupelekwa nchini Uganda na Sudani Kusini pamoja na makambi ya wakimbizi ya Nduta na Nyarugusu yaliyopo mkoani Kigoma.

Naye Kaimu Meneja wa Taasisi ya Kuhifadhi Chakula Kanda ya Dodoma Felix Ndungulu amesema wamefikia hatua ya kuuza Mahindi baada ya serikali kujiridhisha kuwa kwasasa chakula kilichopo nchini kinajitosheleza.