
Ng'ombe wanne wamekufa ,baada ya kudaiwa kupigwa risasi, na askari wa wanyamapori wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kwa madai ya kuingizwa hifadhini kinyume cha sheria.
Diwani wa kata ya Nyanungu, Tiboche Richard, akizungumza kwa njia ya simu amesema ,tukio hilo limetokea wakati askari hao wakiwa katika doria ya kawaida , ambapo walianza kufyatua risasi hovyo, na kuua ng'ombe hao wanne katika kijiji cha Kegonga kata ya Nyanungu wilaya ya Tarime.
