
Viongozi wa mapinduzi nchini Gabon, wamemchagua Jenerali Brice Oligui Nguema, kuwa Rais wa mpito wa nchi hiyo, baada ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumamosi, yaliyomtangaza Bw.Ali Bongo kama mshindi wa Uchaguzi huo.
.
Jenerali Nguema anachukua madaraka hayo huku ikitajwa kuwa ni binamu wa rais aliyeondolewa madarakani.
