Back to top

NHIF YAREJESHA DAWA 178 ZILIZOONDOLEWA

08 May 2024
Share

Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF), umerejesha dawa 178 pamoja na kujumuisha dawa nne zilizokuwepo kwenye mwongozo wa Taifa wa matibabu lakini hazikuwemo kwenye Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (NEMLIST) ambapo umezijumuisha dawa hizo kwenye Kitita chake cha Mafao cha Mwaka 2023.
.
NHIF imeeleza hayo kupitia taarifa yake kwa umma ambapo imeeleza kuwa hatua hiyo inaongeza wigo wa upatikanaji wa dawa kwa wanachama kwa kuzingatia miongozo ya tiba nchini.
.
Kutokana na maboresho hayo, Mfuko wa Taifa Bima ya Afya unawahakikishia wanachama wake kuwa huduma za matibabu zitaendelea kupatikana katika vituo vyote vilivyosajiliwa nchi nzima na endapo kutakuwa na changamoto za kiutekelezaji.
.
Aidha NHIF imevishauri vituo vinavyotoa huduma viwasiliane na ofisi za Mfuko huo kuepuka usumbufu usio wa lazima kwa wateja wao.