Back to top

Nigeria imethibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza wa Corona.

28 February 2020
Share

Waziri wa afya wa Nigeria Osagie Ehanire amesema mgonjwa huyo ni raia wa Italia anayefanya kazi nchini humo na amerejea tarehe 25 ya mwaka huu akitokea Milan nchini Italia.

Hata hivyo, amesema mgonjwa huyo anaendelea vizuri na anatibiwa kwenye hospitali ya magonjwa ya kuambukiza ya Yaba, jijini Lagos.

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema mataifa yote yanatakiwa kujiandaa kukabiliana na virusi vya Corona.

Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Gebreyesus ameelezea wasiwasi wa taarifa zilizotokea nchini Japan za mgonjwa aliyepona kurudiwa upya na maambukizi.