Back to top

NINI HATMA YA RONALDO NA PEPE URENO?

06 July 2024
Share

Kocha wa Ureno Roberto Martinez, amesema hakuna maamuzi yoyote  yaliofanywa mpaka sasa kuhusu mustakabali wa kimataifa wa Cristiano Ronaldo na Pepe, baada ya kushindwa na Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2024 hapo jana.

Hii ni baada ya kuibuka kwa tetesi ya kwamba wawili hao, huenda ikawa ndio mwisho wao kucheza soka la Ureno kutokana na sababu za umri.

Wachezaji hao wawili wamekuwa wakishiriki mara kwa mara katika timu ya Ureno katika muda wote wa michuano hiyo, huku Ronaldo mwenye umri wa miaka 39 akicheza kila dakika ya ushindi wa mikwaju dhidi ya Slovenia, katika hatua ya 16 bora na kushindwa kwa mikwaju ya penalti na Ufaransa katika robo fainali.


Kocha Martinez, alipoulizwa kama wachezaji hao wawili walikuwa wamecheza Ureno kwa mara ya mwisho, Martinez alijibu hapana na kusema kuwa ni mapema sana kulijibia hilo kwani bado wanakabiliana na matokeo mabaya walioyapata.