Back to top

"Nitamkumbuka Prof.Ndulu kwa ushauri wake wa kuimarisha uchumi"-JPM

22 February 2021
Share

Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia na wafiwa wote kufuati kifo cha Gavana Mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Benno Ndulu aliyefariki Februari 22, 2021 katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar Es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Rais Dkt.John Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema atamkumbuka Prof.Benno Ndulu kwa ushauri wake wa kuimarisha uchumi wa nchi hususani mageuzi katika sekta ya fedha. 

Ameongeza kwa kusema marehemu  Prof.Ndulu alikuwa mchapakazi na mnyenyekevu, hivyo Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.