
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo anayedaiwa kujiteka wiki chache zilizopita amefikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa na kusomewa mashtaka mawili likiwemo la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni.
Akisoma Mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Iringa John Mpitanjia wakili wa Serikali Abed Mwandalamo amesema mshitakiwa anashitakiwa kwa makosa mawil, Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa whatsapp kinyume na sheria ya makosa ya mtandao No.16 ya mwaka 2016.
Kosa la pili kutoa taarifa za uongo kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu No.122 sehemu (a) kwa kutoa taarifa kwa mtumishi wa serikali ambaye ni afisa polisi No. E 2328 Koplo Salim akimfahamisha kwamba ametekwa na watu wasiojulikana na kupelekwa kwenye kiwanda cha pareto PCT Mafinga huku akijua kuwa taarifa hiyo ni ya uongo.
Kesi imeahirishwa mpaka jumatatu ya tarehe 26 March 2018 ambapo hakimu atatoa uamuzi kwamba mshitakiwa apewe dhamana ama asipewe dhamana, mshitakiwa amerudishwa rumande.