Back to top

Nyuki wachavushaji hatarini kutoweka Tanzania.

12 March 2019
Share

Wataalamu wa nyuki Tanzania wamesema nyuki wachavushaji wa mimea wako hatarini kutoweka hapa nchini kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na wakulima kutumia kemikali za viwandani msimu wa kilimo.

Mtaalamu wa nyuki Tanzania Dk Hendry Njovu amesema tatizo la uharibifu wa mazingira limethiri kwa kiasi kikubwa nyuki ambao kwa asilimia 90 wanategemewa kwa ajili ya uchavushaji wa mazao ya chakula na biashara.

Amesema nyuki kwa sasa wameanza kupotea dunia na kwamba Uchina kwa sasa wanategemea binadamu kufanya shughuli za uchavushaji jambo ambalo kwa nchi zinazoendelea litakuwa gumu kutokana na kutumia gharama kubwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha usimamizi wanyamapori Mweka Prof Japhary Kidegesho amesema kama hatua za haraka za kuhifadhi nyuki hazitachukuliwa kuna hatari ya nchi kukumbwa na baa la njaa kutokana na wadudu hao wanaotegemewa kwa ajili ya uchavushaji wa mimea na miti kutoweka.