Back to top

Nyumba yenye familia tisa yateketea kwa moto mkoani Mbeya

17 September 2019
Share

Familia tisa zimenusurika kifo na kwa sasa hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi iliyopo mtaa wa Isanga jijini Mbeya kuwaka moto ambao umeteketeza mali zote zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo.

Ni kilio na simanzi kwa wapangaji wa nyumba hii baada ya moto kulipuka na kuteketeza nyumba yao kabla ya jeshi la zimamoto na uokoaji kufika ka kufanikiwa kuudhibiti.

Mmiliki wa nyumba hiyo, Bwana Joseph Michael Mpanji amesema moto huo umesababisha hasara kubwa kwake na wapangaji wake kwa vile vitu vyote vilivyokuwa ndani ya vyumba vya wapangaji wake vimeteketea.