Back to top

O YEONG-SU WA SQUID GAME, ASHTAKIWA KWA UNYANYASAJI WA KINGONO

28 November 2022
Share

Mwigizaji wa tamthilia ya Squid Game, O Yeong-su mwenye umri wa miaka 78, amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono, ambapo anatuhumiwa kumgusa isivyofaa mwanamke mmoja mwaka 2017.
.
Kufuatia shtaka hilo, Wizara ya Utamaduni ya Seoul imeripotiwa kuacha kurusha matangazo ya serikali yanayomuhusisha mwigizaji huyo.
.
Hata hivyo Bw. O Yeong-su amekanusha mashtaka hayo.