Back to top

Ocean Viking yawaokoa wahamiaji 196 kutoka bahari ya Libya.

01 August 2021
Share

Meli ya msaada ya Ocean Viking imewaokoa wahamiaji 196 kutoka bahari ya Libya.

Shirika la msaada la Ulaya la SOS Mediterranee limesema meli hiyo kwanza iliwaokoa watu 57 kutoka boti moja lililokuwa likiyumbayumba katika bahari ya taifa hilo.

Wakati wa mchana, wafanyakazi wa meli hiyo, walifanya uokoaji mwingine wa ziada katika eneo hilo hilo na kuwakoa watu 54 kutoka kwa boti nyingine na wengine 64 kutoka kwa meli ya mbao.

Watu jumla waliookolewa ni pamoja na wanawake wawili wajawazito na watoto 33 ambao 22 kati yao hawakuwa wameandamana na mtu.

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa, limesema kuwa kiasi cha watu 1,146 wamekufa baharini wakijaribu kufika Barani Ulaya wakati wa nusu ya kwanza ya mwaka 2021.