
Kampuni ya Smartmatic ya nchini Uholanzi iliyotumika kutoa huduma ya kiteknolojia kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya imekataa kufungua server za Tume hiyo ikidai kuwa sheria zake haziruhusu licha ya mahakama kuu nchini humo kuagiza server hizo zifunguliwe ili walalamishi wafanye ukaguzi.
