Back to top

Odinga apinga matokeo ya uchaguzi, Kenya

16 August 2022
Share

Kiongozi wa Muungano wa Azimio nchini Kenya, Raila Odinga amepinga matokeo ya uchaguzi uliomtangaza Naibu wa Rais William Ruto kuwa ndiye Rais Mteule, kwasababu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Bw.Wafula Chebukati alikiuka katiba kabla ya kumtangaza mshindi.
.
Raila Odinga amesema makamishna wa tume hiyo hawakukubaliana kuhusu hesabu ya mwisho ya matokeo hayo yaliyompatia ushindi William Ruto.
.
Hata hivyo, Odinga amewataka wafuasi wake kudumisha amani na utulivu huku muungano huo ukifuata njia za kikatiba za kubatilisha matamshi ya Bw Chebukati.